HabariMilele FmSwahili

Edith Nyenze ndiye mbunge mpya wa Kitui Magharibi

Edith Nyenze ndiye mbunge mpya wa Kitui Magharibi. Bi Nyenze wa chama cha Wiper, ameibuka mshindi katika uchaguzi wa jana kwa kura elfu 14, 372. Dennis Muli Mulwa, mwaniaji huru ameshikilia nafasi ya pili kwa kura 2,046 akifuatiwa na wake mkuu Robert Mutiso Leli wa NARK Kenya ambaye amezoa kura elfu 1,784. Fridah Nyiva Mutui wa Kenya National Congress ameibuka wa nne kwa kura 1,075, naye Elijah Muimi Kilonzi akipata kura 499. Matokeo hayo yamedhibitishwa na afisa aliyesimamia uchaguzi huo James Mbai. Bi. Nyenze akiwarai wapinzani wake kushirikiana naye katika kukamilisha miradi aliyoasisi mumewe marehemu Francis Nyenze.

Show More

Related Articles