HabariMilele FmSwahili

Waziri Keriako Tobiko kuzuru msitu wa Kakamega leo

Waziri wa misitu Keriako Tobiko anatarajiwa kuzuru msitu wa Kakamega na kupanda miche 16 000 ya miti asubuhi hii. Afisa wa misitu jimbo la Kakamega Martin Wandabwa amesema wako na mpango  wa kupanda zaidi ya miche laki nane msimu huu wa mvua kuhakikisha wanafiki kiwango cha asilimia kumi ya upanzi wa miche kinachohitajika. Wandabwa amesema mpango utashirikisha jamii zinaoishi karibu na misitu na hasa wanalenga maeneo yaliyokatwa miti zilizokuwa zimefikisha miaka ya kukatwa.

Show More

Related Articles