Mediamax Network Limited

Reli Ya Kisasa Yatajwa Kuimarisha Biashara Miritini Mombasa.

Wafanyibiashara eneo la Miritini hapa Mombasa wameeleza kunawiri kwa biashara zao pakubwa kutokana na ujio wa reli  mpya ya kisasa.

Baadhi tuliozungumza  nao wanasema wateja wamekuwa wengi tangu kuanzishwa kwa mradi huo.

Wanasema hali ya maisha pia imeimarika ikiwemo uuzaji wa ardhi katika maeneo hayo, hali ambayo pia imewasaidia pakubwa kujikimu kimaisha.

Hata hivyo baadhi wameonyeshwa kutoritdhishwa na hatua ya kuongezwa kwa nauli ya gari moshi wakisema huenda ikamwathiri pakubwa mwananchi wa kawaida.

Wengine wameunga mkono kuongezwa kwa nauli kutoka shilingi 700 hadi elfu moja kwa wasafiri wa kitengo cha kwanza.