HabariSwahili

Shule ya Msingi ya Mlolongo yafungwa kufuatia nyufa madarasani

Shule ya msingi ya Mlolongo kaunti ya Machakos imefungwa mara moja kufuatia nyufa kubwa kubwa kutani.
Shule hiyo ilijengwa na mamlaka ya barabara kuu nchini KENHA, kufuatia upanuzi wa barabara ya Nairobi kuelekea Mombasa.
Itabidi wanafunzi elfu moja wa shule hiyo kuelekea nyumbani hadi KENHA itakapomaliza kujenga madarasa ya muda.
Hii leo kamishna wa kaunti ya Machakos Matilda Sakwa, pamoja na viongozi kutoa wizara ya elimu na wengineo walifika na kuthibitisha kufungwa kwake.

Show More

Related Articles