HabariSwahili

Mhudumu wa duka la MPESA ashtakiwa kwa kuhusika katika ulaghai

Mwanamke mmoja kwa jina Catherine Nyaboke anayefanya kazi katika duka la Mpesa hii leo amewasilishwa katika mahakama ya Milimani ili kujibu mashtaka matano dhidi yake ya kushirikiana na mwanamume anayefahamika kama Benson Waziri Masubo Chacha kwa kosa la kusajili nambari ya simu kwa jina la mwakilishi wa wanawake wa Muranga, Sabina Chege ili kuwalaghai wabunge.
Aidha kama mwanahabari wetu Grace Kuria anavyotueleza, mshtakiwa aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki mbili au shilingi laki moja pesa taslimu.
Polisi wangali wanamsaka mshukiwa mkuu.

Show More

Related Articles