HabariPilipili FmPilipili FM News

Edith Nyenze Anaimani Kushinda Ubunge Wa Kitui Magharibi.

Wakazi wa kitui magharibi leo wanashiriki uchaguzi mdogo kuchagua mbunge mpya, kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa eneo hilo Francis Nyenze.

Zoezi la uchaguzi limeng’oa nanga kuanzia saa kumi na mbili unusu huku usalama ukiwa umeimarishwa katika vituo vyote 143 eneo hilo.

Kati ya wanao wania wadhfa huo ni mjane Edith Nyenze ambaye anawania kiti hicho kwa tiketi ya wiper, huku mpinzani wake mkuu Elijah Muimi Kilonzi akiwania wadhfa huo kwa tiketi ya chama cha muungano.

Akiongea mda mfupi tu baada ya kupiga kura yake Edith Nyenze ameleza imani yake ya kuibuka mshindi katika zoezi hilo.

Wengine ni Robert Mutiso wa chama cha NARC Kenya, Fridah Nyiva wa chama cha National Congress, na mgombea huru Denis Muli Mulwa.

Show More

Related Articles