MichezoPilipili FmPilipili FM News

Wanyama Kuikosa Mechi Ya Kirafiki Dhidi Ya Jamhuri Ya Kati.

Nahodha wa kikosi cha timu ya taifa Harambee Stars Victor Mugubi Wanyama hatakuwepo kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya kati ambayo itatandazwa tarehe 27 mwezi huu nchini Moroco katika uwanja wa Stade de Marrakech.

Kiungo huyo amejiunga na timu yake ya Tottenham ya Uingereza hii ni baada ya kilabu hio kukubaliana na shirikisho la soka FKF kuwa Wanyama angehusika kwa mechi moja tu dhidi ya Comoros.

Wanyama alifunga bao moja kwa njia ya penati dhidi ya Comoros ambapo mechi hio ilitoka sare ya 2-2.

Tottenham itakabiliana na Chelsea wikemdi ijayo na Wanyama anatarajiwa kuanza kwenye mechi hio mhimu ambayo itaamua kama watamaliza ndani ya nne bora ili kufuzu kwa ligi ya kilabu bingwa barani ulaya.

Show More

Related Articles