Mediamax Network Limited

Safaricom kutatiza huduma zake wiki hii kwa ajili ya ukarabati

Kampuni ya Safaricom itakatiza huduma zake wiki hii kwa ajili ya ukarabati. Kampuni hiyo imesemja kuwa huduma za kujaza salio huduma za Okoa jahazi, kutuma ujumbe mfupi na kupiga simu nje ya nchini ni miongoni mwa zitakazo katizwa kati ya saa tatu asubuhi siku ya Jumatano hadi saa sita unusu usiku wa kuamkia Alhamisi. Mkurugenzi wa kupanga mikakati Joseph Ogutu amesema hatua hiyo itawezesha Safaricom kuzindua huduma bora za kisasa kwa wateja wake milioni 29 nchini.