HabariMilele FmSwahili

Upigaji kura kubaini atakayekuwa mbunge wa Kitui Magharibi waendelea

Upigaji kura unaendelea wakati huu kubaini ayakayekuwa mbunge mpya wa Kitui Magharibi. Wapigaji kura wanaendelea kumiminika katika vituo huku idadi yao ikiripotiwa kuwa ndogo. Wadhifa huo uliosalia wazi Disemba mwaka jana kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge Francis Nyenze umewavutia wagombeaji watano akiwemo mkewe marehemu edith Nyenze wa chama cha Wiper ambaye anapigiwa upato kutwaa wadhfa huo. Afisa wa IEBC ayesimamia zoezi ili Paul Kurgat anasema hawatapeperusha matangazo ya matokeo ya kura moja kwa moja, kama ilivyokuwa miaka ya awali bali watatangaza matokeo ya mwisho pekee.

Show More

Related Articles