HabariMilele FmSwahili

Noordin Kaji kuhojiwa leo hili kujaza nafasi ya mkurugenzi wa mashitaka ya umma

Naibu mkurugenzi wa idara ya ujasusi Noordin Haji anahojiwa leo baada ya kupendekezwa na rais Kenyatta kuwa mkurugenzi wa mashitaka ya umma. Hajji ameratibiwa kufika mbele ya kamati ya bunge ya maswala ya kisheria saa tatu unusu asubuhi hii. Hajji aliibuka bora kwenye orodha ya wawaniaji waliojumuishwa manaibu wa kiongozi wa mashitaka Dorcas Oduor na Jacob Ondari na wakili Lucy Kambuni. wakati uo huo kamati za bunge pia zitawahoji makatibu wa wizara wateule john morangi wa wizara ya uchimbaji madini na alfre korir wa magereza. Wengine ni Jerome Ochieng wa wizara ya habari na teknolojia Harry Kimtai wa mifugo na Susan Koech wa wizara ya Afrika Mashariki.
Yakijiri hayo kamati ya bunge kuhusu maswala ya kigeni itawapiga msasa mabalozi wanne wateule Richard Titus Ekai John Okuna Ogango Wilfred Gisuka Machage na Mohamed Muktar Shidiye

Show More

Related Articles