BurudaniPilipili FmPilipili FM News

Bawazir Akanusha Kukosana Na Meneja Wake.

“Mimi sioni tatizo tuko sawa na Bawzir na kukinzana kuko ila si kama vile watu wanavyoweka chumvi katika swala hilo”. Amesema Babaz

Baada ya kukosana na msanii Chikuzee meneja maarufu Musa Babaz alibadilisha dira na kuanza kumsimamia The City Boy maarufu kama Bawazir lakini ndo ya wawili hao inaonekana kuanza kuyumba hii ni baada ya msanii huyo kurudia kosa alilolifanya Chikuzee la kuachilia ngoma kabla ya meneja wake kupeana ruhusa.

Akihojiwa kupitia njia ya simu kwenye kipindi cha Zinduka ndani ya pilipili fm Musa Babaz ameonekana kukanusha swala hilo ila katika mahojiano hayo Babaz pia alionekana kama kukubali kuwa mambo hayako sawa ila akadokeza ni kawaida na mambo yako sawa.

“Mimi sioni tatizo tuko sawa na Bawzir na kukinzana kuko ila si kama vile watu wanavyoweka chumvi katika swala hilo”. Amesema Babaz.

Bawazi aliachilia ngoma yake mpya aliyoibandika jina Shuga Mummy ambayo iliambatana na Video kwa mkupuo, ngoma hio inaendelea kufanya vizuri kwa sasa.

Kwa upande wake msanii Bawazie amekanusha kuwa na issue na meneja wake akisema wako sawa na wanapanga kudondosha ngoma nyengine kali baada ya shugs mummy so mafans wake wasubiri vitu vikubwa.

Lakini hapa tatizo kubwa linaonekana ni pale msanii alipoachilia video bila ya meneja kujua but wote wamekanusha kuwepo kwa mzozo na wakahakikisha wako pao na kazi zitakuja mob sana.

Show More

Related Articles