HabariMilele FmSwahili

Gavana Sang apendekeza walimu wa chekechea kuajiriwa na TSC

Gavana wa Nandi Stephen Sang sasa anapendekeza waalimu wa chekechea kuajiriwa na tume ya TSC. Akizungumza alipokukatana na maafisa kutoka wizara ya elimu, anasema kaunti zinafaa kuachiwa jukumu la kuboresha miundo msingi shuleni. Sang kadhalika amefurahia hatua ya wizara hiyo kukusanya maoni ya wadau mbalimbali kuhusiana na mageuzi yanayoendelea. Katibu katika wizara hiyo Belio Kipsang, akizungumza alipozuru kaunti hiyo, alitoa hakikisho kuwa wadau wote watashirikishwa kikamilifu kwenye mageuzi hayo.

Show More

Related Articles