HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Gavana Sonko na Waziri Macharia wafokewa kwa miundo msingi duni jijini

Rais Uhuru Kenyatta hii leo ameagiza gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko, na waziri wa uchukuzi wa umma James Macharia kuimarisha miundo msingi jijini, akisisitiza kuwa wenyeji wa jiji wamechoka na usumbufu wa mafuriko barabarani na mitaani.
Kulingana na rais kama alivyoahidi Sonko kwenye kampeni zake, sharti atimize, na wakati ni sasa.
Aidha amempa changamoto waziri wa uchukuzi wa umma kuwa anapswa kufanya kazi na gavana Sonko, na kuhakikisha kuwa ujenzi wa barabara za jiji umekamilika.

Show More

Related Articles