HabariMilele FmSwahili

Mbunge Omar Mohammed aondoa hoja ya kubanduliwa waziri Kariuki bungeni

Mbunge wa Mandera mashariki Omar Mohammed ameondoa hoja aliowasilisha bungeni kutaka waziri wa afya Sicily Kariuki kubanduliwa. Kiongozi wa wengi bungeni Aden Duale anasema uamuzi huo umeafikiwa kuruhusu lalama zilizoibuliwa na wabunge kutatuliwa na uongozi wa chama cha Jubilee.
Aidha,Mohammed amekana kushawishiwa kuondoa hoja hiyo akisema alichukua hatua hiyo baada ya mashauriano ya kina na wakuu wa Jubilee.

Show More

Related Articles