HabariPilipili FmPilipili FM News

Walimu Kutoka Eneo La Kaskazini Wakutana Na Kamati Ya Bunge.

Walimu kutoka kaskazini mashariki mwa nchi wamefika mbele ya kamati ya elimu bungeni kuelezea changamoto wanazopitia wakiwa kazini eneo hilo.

Baadhi ya walimu hao wanasema licha ya kuwasilisha malalamishi yao mbele ya tume ya kuajiri walimu TSC wakitaka uhamisho hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

Nao maafisa wa tume ya kitaifa ya kutetea haki za binadamu wanasema lazima malalamishi ya walimu hao yashughulikiwe kwani yameathiri pakubwa elimu katika shule za eneo hilo ikizingatiwa kuwa hakuna masomo yanayoendelea.

Kamati hiyo ianyoongozwa na mwenyekiti Wilson Sossion inaedelea kujadili hoja hiyo akisema suluhu itapatikana.

Haya yanajiri baada ya walimu hao kudai ukosefu wa usalama, huku walimu wakike wakilazimika kulipa ada Fulani kwa kukataa ofa ya kuolewa na mwalimu mkuu.

Show More

Related Articles