HabariPilipili FmPilipili FM News

Jaji Kihara Apigwa Msasa.

Jaji Paul Kihara Kariuki amefika mbele ya kamati ya uteuzi bungeni ili kukaguliwia kujaza nafasi ya mwanasheria mkuu.

Akijieleza, amesema uzoefu alionao kama jaji utahakikisha anatekeleza majukumu yake kama mkuu wa sheria iwapo ataidhinishwa.

Pia ameahidi kwamba atahakikisha asasi tatu za serikali zinafanta kazi pamoja.

Amekiri kwamba hapo awali idara hizo  za serikali zimekua zikilumbana.

Kihara alipendekezwa na rais kuchukua wadhfa huo baada ya kujizulu kwake Githui Muigai.

Show More

Related Articles