HabariMilele FmSwahili

Rais kuzindua awamu ya pili ya ujenzi wa bara bara ya kisasa ya Ngong leo

Rais Kenyatta asubuhi hii atazindua awamu ya pili ya ujenzi wa bara bara ya kisasa ya Ngong hapa jijini Nairobi. Ujenzi wa bara bara hiyo kutoka eneo la Prestige Hafi Dagoreti Corner unafadhiliwa na serikali ya Japan kwa kima cha shilingi bilioni 2.2. aidha bara bara hiyo yenye umbali wa kilomita 3.4 itakamilika mwaka 2019 na inatarajiwa kupunguza msongamano wa magari.

Show More

Related Articles