HabariMilele FmSwahili

Serikali yakanusha kuagiza kufungwa kwa baa zote nchini

Serikali imekanisha madai ya kuagiza kufungwa kwa baa zote nchini katika jitihada za kukabili biashara ya pombe haramu. Katika taarifa msemaji wa wizara ya usalama Mwenda Njoka ametaja kuwa uvumi madai kuwa waziri dkt Fred Matiangi aliagiza kufungwa baa zote wakazi wa ziara yake kaunti ya Kiambu. Njoka amesisitiza kujitolea kwa serikali kuwalinda wauzaji vileo wanaozingatia sheria dhidi ya kuhujumiwa.

Show More

Related Articles