HabariMilele FmSwahili

Tobiko :Maafisa wa misitu wanaojihusisha na ufisadi na utendakazi duni watafutwa kazi

Maafisa zaidi wa misitu wanaojihusisha na ufisadi na utendakazi duni watafutwa kazi. Waziri wa mazingira Keriako Tobiko anadai kukithiri uovu katika shirika la uhifadhi wa misitu na hivyo kuathiri lengo la serikali kuafikia upanzi zaidi wa miti. Akizugumza katika msitu wa Karura alikooongoza hafla ya kuadhimisha siku ya upanzi wa miti,Tobiko anasema serikali imejipnga kuafikia asilimia 10 ya misitu nchini ifikiapo mwaka 2022.

Upanzi huo wa miti pia umeshuhudiwa kaunti ya Garissa, wanafunzi na wanaharakati wakiugana kupanda miti katika msitu wa Boni

Kaunti ya Kiambu wenyeji wakijitokeza kupanda miche za miti katika baadhi ya misitu eneo hilo

Kaunti ya Nakuru spika wa bunge la kaunti hiyo Mhandisi Joel Kairu amesema wananuia kufanikisha upanzi wa miti milioni 30 kaunti hiyo wakitoa wito kwa wenyeji kuwaunga mkono.

Show More

Related Articles