HabariPilipili FmPilipili FM News

Hofu Ya Simba Yatanda Ganze Kilifi.

Hofu imewazonga wananchi wa Mrima wa Ndege kaunti ndogo ya Ganze baada ya simba kuvamia kijiji cha Gumara na kuua ngombe wawili mapema leo asubuhi.

Walioshuhudia kisa hicho wamesema kuwa simba huyo amevamia ngombe hao katika boma lao jambo ambalo limepelekea wananchi kujitokeza ili kukabiliana na mnyama huyo.

Hamphrey Safari mmoja wa wananchi hao amesema kuwa simba huyo ametorokea msituni na kwa sasa wananchi hao wanaishi kwa hofu ya kuvamiwa.

Wananchi hao sasa wanalitaka shirika la wanyama pori nchini kuingilia kati ili kuhakikisha kuwa simba huyo amerudishwa kwenye mbuga za wanyama.

Mapema mwaka huu mwanamme mmoja alivamiwa na kujeruhiwa vibaya na chui katika kijiji cha Kidemu katika eneo la Bamba.

Show More

Related Articles