HabariPilipili FmPilipili FM News
Mwashetani Ataka Wakata Miti Lungalunga Kukabiliwa Vikali.

Mbunge wa Lungalunga kaunti ya Kwale Khatib Mwashetani ameitaka serikali kupitia wizara ya misitu kuchunguza ukataji wa miti na uchomaji makaa unaoendelezwa katika eneo hilo licha ya uchomaji makaa kupigwa marufuku hivi majuzi na naibu rais William Ruto.
Mwashetani amesema eneo la lungalunga limekuwa maficho ya wafanyibiashara wa makaa kutoka kaunti mbalimbali ambako marufuku ya makaa inatekelezwa kikamilifu.
Amesema zaidi ya lori 10 kila siku husafirisha makaa kutoka eneo la Lungalunga.