HabariMilele FmSwahili

Wabunge wamtaka Kavuludi kung’atuka afisini kwa kigezo cha utendakazi duni

Wabunge sasa wanamtaka mwenyekiti wa tume ya huduma za polisi Johnstone Kavuludi kung’atuka afisini kwa kigezo cha utendakazi duni. Wakijadili hoja kuhusu mazingira ya kufanyia kazi kwa maafisa wa polisi,wabunge wakiongozwa na kiongozi wa wachache John Mbadi wamemshtumu Kavuludi kwa kutoangazia maslahi ya polisi hasa wanaofanya kazi katika maeneo ya mbali. Wamesema wakati umefika tume ya polisi kuwa na wakuu wapya watakaohakikisha polisi wanalipwa vizuri na kuishi katika nyumba za kisasa.

Show More

Related Articles