HabariMilele FmSwahili

Rais Uhuru aelekea nchini Rwanda kwa ziara rasmi

Rais Uhuru kenyatta amesafiri nchini Rwanda kujumuika na wakuu wengine wa Afrika kwenye hafla ya utiaji sahihi maafikiano kuhusu eneo huru la kibiashara. Mkakati huo unatarajiwa kufanikisha mpango wa kukuza bara hili kiviwanda na kiuchumi. Aidha biashara baina ya nchi za Afrika itakuwa kutoka kiwango cha sasa cha asilimia 13 na kuwavutia wawekezaji zaidi. Rais Kenyatta Paul Kagame wa Rwanda na Yoweri Museveni wa Uganda wamehusika pakubwa katika kuhimiza kubuniwa eneo huru la kibiashara Afrika. Wakuu wa nchi 27 wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huu

Show More

Related Articles