HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Kamati ya afya bungeni yapendekeza kamati mpya kubuniwa

Kamati ya afya bungeni ikiongozwa na mwenyekiti Sabina Chege ambayo imekuwa ikichunguza masihara ya upasuaji katika hospitali ya kenyatta hii leo imependekeza bodi mpya ibuniwe katika hospitali kuu ya Kenyatta.
Kamati hiyo imependekeza kwamba bodi mpya itakayobuniwa iwachunguze afisa mkuu mtendaji Lily Koros ambaye yuko kwenye likizo ya lazima pamoja na mkurugenzi wa huduma za kliniki Benard Githae kujua iwapo wamehitimu kuendelea kushikilia nyadhifa hizo au wapigwe kalamu.
Ripoti hiyo inatarajiwa kuwasilishwa bungeni hiyo kesho kujadiliwa.

Show More

Related Articles