HabariMilele FmSwahili

James Orengo ndiye kiongozi wa wachache katika bunge la seneti

James Orengo ndiye kiongozi wa wachache katika bunge la seneti. Spika Ken Lusaka amemuidhinisha Orengo baada ya kupokea mabadiliko hayo kutoka kwa masenta wa NASA. Orengo amechukua wadhifa huo kutoka kwa Moses Wentagula baada ya maseneta 19 kati ya 28 wa NASA kukubaliana kumtimua Wetangula. Naibu wa Orengo sasa ni seneta wa Kakamega Cleophas Malala.

Idhinisho hili linalowadia huku kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka akimtaka Orengo kutokubali uteuzi huo. Akiongea baada ya kuongoza kikao cha wabunge wa Wiper, Kalonzo ameonya iwapo Orengo atakubali wadhifa huo basi atachangia kusambaratika NASA.

Usemi wa Kalonzo umeungwa mkono na kinara wa ANC Musalia Mudavadi anayesema hawatakubali jaribio lolote la kumbandua Wetangula kama kiongozi wa wachache.

Show More

Related Articles