HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Wetangula atajua hatma kesho iwapo ataondolewa kuwa kiongozi wa wachache

Kiongozi wa chama cha Wiper na mmoja wa vinara wa muungano wa Nasa Kalonzo Musyoka amesema kuwa seneta wa Bungoma ambaye ndiye kiongozi wa wachache kwenye bunge la senate hatapokjonywa kwa vyovyote vile wadhifa wake kama kiongozi wa waliowachache kwenye bunge la senate.
Usemi huu alioibua akiwa Kitui leo kwenye kampeni za chaguzi ndogo za jumatatu ijayo kwenye eneo bunge la Kitui West umewadia huku mkutano wa maseneta wanaogemea upande wa chama cha ODM kwenye bunge la seneti ukikosa kufanyika leo kama ulivyokuwa umetaratibiwa na inakisiwa kuwa utaandaliwa kesho saa tatu asubuhi ili kutoa mwelekeo kuhusiana na agizo alilotoa spika siku ya Alhamisi kuhusiana na suala hilo.

Show More

Related Articles