HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosTop StoriesVideos

Tume ya huduma za polisi yakana maafisa zaidi ya 1000 wamejuizulu

Mwenyekiti wa tume ya huduma za polisi Johnstone Kavuludi amepuuzilia mbali ripoti kwamba takriban maafisa wa polisi elfu moja wamejiuzulu hivi karibuni kwa kuwa mishahara yao inalengwa kupunguzwa.
Kavuludi badala yake amesema tume hiyo inafanya ukaguzi wa stakabadhi za maafisa wa usalama na kuwa kila mmoja atalipwa kulingana na stakabadhi zake za kimasomo na ujuzi.
Haya yanajiri wakati mawakili wa polisi Prof. George Wajackoyah na Nelson Havi wanapania kuelekea mahakamani kwa kile wanachotaja kuwa unyanyasaji kwa polisi.

Show More

Related Articles