HabariPilipili FmPilipili FM News

Serikali Yahimizwa Kutatua Visa Vya Ubakaji Taita.

Mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Taita Taveta Lydia Haika ameitaka serikali ya kitaifa kuingilia kati na kutatua kero la  visa vya wanawake kubakwa.

Haika amesema sasa wanawake katika kaunti hiyo wanaishi kwa hofu kwani hata sasa hakuna hata mshukiwa aliyetiwa mbaroni kuhusiana na visa hivyo.

Sasa Haika ameiomba serikali ya kitaifa kuanzisha kitengo cha kuwasaidia waathirika wa dhuluma maarufu (rescue centre) ambapo watapokea ushauri.

Wakati huo huo Haika amempongeza gavana Samboja kwa juhudi zake kupigana na utumizi wa pombe haramu miongoni mwa vijana.

 

Show More

Related Articles