HabariPilipili FmPilipili FM News

Mwanamume Asombwa Na Maji Malindi.

Mwanaume mmoja amepatikana kando ya mto Galana akiwa amefariki mapema leo baada ya kusombwa na maji katika eneo la Lango Baya kaunti ndogo ya Malindi.

Kulingana na wakaazi wa eneo hilo, mwaume huyo alitoweka jana huko Lango Baya baada ya kusombwa na maji alipokuwa akiendeleza shughuli za ukulima.

Akithibitisha kisa hicho naibu chifu wa eneo hilo Steven Gunga amesema mwili wa marehemu umepatika baada ya wakaazi kujaribu kumtafuta usiku kucha.

Aidha Gunga amewataka wakaazi kuwa makini wakati huu wa mafuriko akisema kuwa huenda mafuriko hayo yakazidi kushuhudiwa hata zaidi katika siku za usoni.

Mwili wa marehemu umepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti kwenye hospitali kuu ya Malindi.

 

Show More

Related Articles