HabariPilipili FmPilipili FM News

Washukiwa 5 Wa Wizi Mombasa Wafikishwa Mahakamani.

Washukiwa watano waliokamatwa na kushtakiwa kwa kosa la kuwawekea vileo watu kwenye vinywaji, na kisha kuwapora eneo la Mtwapa Kaunti ya Kilifi, wamefikishwa katika mahakama ya Shanzu hii leo.

Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Diana Mochache watano hao akiwemo mwanamume mmoja, wamekana mashtaka dhidi yao.

Hakimu Mochache aidha ameridhia ombi la upande wa mashtaka la kutaka muda wa siku tatu kuwachunguza watano hao.

Kesi hiyo itatajwa tena ijumaa wiki hii huku washukiwa hao wakiendelea kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Mtwapa.

Show More

Related Articles