HabariPilipili FmPilipili FM News

Waziri Balala Azindua Rasmi Kamati Itakayoshughulikia Utalii.

Waziri wa utalii Najib Balala amezindua kamati mpya itakayofanya utafiti ili kuboresha idadi ya watalii wanaokuja nchini kutoka  milioni 1.2 hadi milioni 3 Kwa mwaka.

Akizungumza na wanahabari katika mkutano na wanakamati hao, Balala amesema lengo la utafiti huu ni kuboresha sekta ya utalii Kwa ujumla Kwa kuhakikisha usalama ,miundo msingi na bidhaa za nchi hii zinavutia ikilinganishwa na nchi nyingine.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati hiyo Jennifer Barasa amesema wanafanya ushirikiano na wizara ya utalii kuhakikisha wanaziba pengo zinazochangia watalii kutokuja kwa wingi humu nchini.

Haya yamejiri kwenye kongamano la siku tatu kaunti ya Mombasa linalopania kufanya utafiti wa kina kuboresha sekta ya utalii.

Show More

Related Articles