HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Raila atetea uamuzi “mgumu’’ wa kushirikiana na Rais

Kinara wa NASA Raila Odinga amefichua kuwa haikuwa rahisi kwake kukubali kuzungumza na rais Uhuru Kenyatta, na kwamba ilimchukua muda kabla ya yeye kuketi meza moja na rais kuzungumza hadi kutia sahihi mkataba wa kufanya kazi pamoja huku naibu rais William Ruto akizidi kutetea hatua ya Odinga.
Haya yalijiri huku vinara wenza wa NASA Kalonzo Musyoka na Musalia Mudavadi wakipinga kubanduliwa kwa kinara mwenza Moses Wetangula kama kiongozi wa wachache kwenye seneti wakiapa kuhakikisha Wetangula anasalia kwenye wadhifa huo.
Kama anavyoarifu Daniel Kariuki siasa zimeonekana kuchukuwa mkondo upya huku duru za kuaminika zikidokeza kuwa Odinga ashaanza kujipanga kuunda mrengo mpya.

Show More

Related Articles