HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Bodi ya madaktari yatoa ripoti yake kuhusu upasuaji tatanishi

Bodi ya ya madaktari ya KMPDB imetoa ripoti kamili kuhusu masihara ya upasuaji katika hospitali kuu ya rufaa ya Kenyatta kwa mgonjwa asiyefaa.
Ripoti hiyo inasisitiza kuwa kosa kuu lililotokea katika kumtayarisha mgonjwa, na hivyo kumuondolea lawama daktari aliyefanya upasuaji huo.
Sasa macho yote yanaelekezwa kwake Mary Nyambura Wahome, muuguzi anayedaiwa kumtayarisha mgonjwa huyo ambaye hakupaswa kufanyiwa upasuaji.
Hii leo, kwenye kikao na kamati ya bunge kuhusu afya, waziri wa afya sicily kariuki, amejitetea na kusema, kuwa kumpa likizo ya lazima afisa mkuu mtendaji wa Kenyatta, Lily Koros, kuliambatana na sheria za uajiri za hospitali kuu ya Kenyatta.

Show More

Related Articles