HabariMilele FmSwahili

Muuguzi alaumiwa kwa upasuaji wa kimakosa KNH

Mary Wahome, muuguzi katika hospitali ya Kenyatta amelaumiwa kutokana na upasuaji wa kimakosa wa ubongo uliofanyiwa mgonjwa. Haya yamebainishwa na bodi ya madaktari , iliyokwua ikichunguza kisa hicho. Anadaiwa kuchanganyikiwa wakati wa kuwapeleka wagonjwa kwenye chumba ha upasuaji.
Hata hivyo madaktari waliohusishwa na upasuaji wa ubongo kimakosa hospitalini Kenyatta, wameondolewa lawama. Kioko anaema daktari mkuu wa upasuaji pamoja na msaidizi wake walifuata taratibu zote zinazofaa kabla ya kufanya upasuaji huo.
Akiwa mbele ya kamait ya bunge kuhusu afya, waziri wa afya Sicily Kariuki amsema ripoti ya bodi hiyo itaamua iwapo Lily Koros atarejeshwa katika usimamizi wa hospitali hiyo kama afisa mkuu mtendaji au la.

Show More

Related Articles