HabariMilele FmSwahili

Wamiliki majengo jijini Nairobi wapewa ilani ya siku 30 kupaka rangi upya majengo yao

Wamiliki majengo jijini Nairobi wamepewa ilani ya siku 30 kupaka rangi upya majengo yao. Katibu wa kaunti Leboo Ole Morintat maafisa wa kaunti watakagua majengo yote kuhakikisha agizo hilo limetekelezwa. Aidha serikali ya kaunti imetishia kuwachukulia hatua wamiliki watakaokiuka agizo. Kwa mujibu wa sheria za kaunti Majengo yanapaswa kupakwa rangi upya kila baada ya miaka miwili ili kutimiza viwango stahiki vya kiafya. Ilani hiyo aidha inafuatia hatua ya gavana Mike Sonko kuanzisha mpango wa kugeuza sura ya jiji la Nairobi ili kuwavutia wawekezaji zaidi.

Show More

Related Articles