HabariMilele FmSwahili

Raia 3 wa Tanzania wanaswa na kilogramu 30 za heroin Mombasa

Raia watatu wa Tanzania wanazuiliwa mjini Mombasa kwa tuhuma za ulanguzi wa mihadarati. Washukiwa hao wanadaiwa kuingiza nchini kilogramu 30 za Heroin zenye thamani ya shilingi milioni 90 kupitia mpaka wa Lunga Lunga. Walinaswa kwenye basi lililokuwa likielekea mjini Mombasa. Aidha kulingana na polisi walikuwa wamepakia dawa hizo kwenye mabegi. Mkuu wa kitengo cha kukabiliana na mihadarati Khamis Massa amesema washukiwa hao wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha bandari. Anasema jamaa hao ni miongoni mwa washukiwa wakuu wa ulanguzi wa mihadarati ambao wamekuwa wakisakwa katika eneo la Pwani.

Show More

Related Articles