HabariPilipili FmPilipili FM News

Shughuli Za Uchukuzi Zarejea Kawaida Katika Barabara Kuu Ya Nairobi-Mombasa

Shughuli za uchukuzi zimerejea kawaida katika barabara kuu ya mombasa-Nairobi, eneo la Kamulu Athiriver ambapo daraja lilifunikwa na mafuriko ya mvua inayonyesha.

Hali ilichangia barabara hiyo kufungwa kwa mda na kulemaza kabisa uchukuzi pamoja na kusababisha msongamano mkubwa wa magari katika pande zote mbili za barabara hiyo.

Mamlaka ya barabara kuu nchini imeleza kukarabati daraja hilo, ambapo sasa ni salama kwa wenye magari kulitumia.

Hayo yakijiri zaidi ya watu 11 wameripotiwa kufariki na mali ya maelfu ya pesa kuharibiwa, huku watu wengi wakipoteza makazi yao kutokana na mafuriko ya mvua inayonyesha nchini.

Aidha Idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini imetabiri uwezekano wa mvua kuendelea kunyesha na kutahadharisha wananchi kusalia wangalifu

Show More

Related Articles