HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Watu 8 wafariki baada ya kusombwa na mafuriko sehemu tofauti

Watu wanane wamethibishwa kufariki, kufuatia mafuriko yanayoshuhudiwa nchini.

Watano waliaga walipokuwa wanasafiri kwenye lori lililokuwa limebeba makaa kaunti ya Kitui, baada ya lori hilo kusombwa na maji.

Aidha wengine watatu waliaga katika kaunti ya Kajiado.

Shule mbili pia ikiwemo shule ya msingi na ile ya upili ya Isinya zimefungwa kajiado, huku ialani ikitolewa kwa shule zilizo maeneo yaliyo karibu na mito, kufunga mara moja.

Jijini Nairobi, magari kadhaa yalisombwa na magari, huku jengo moja likiporomoka juja kaunti ya Kiambu.

Show More

Related Articles