HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Kiambu kutumia 160M kujenga mkahawa wa wawakilishi wadi

Bunge la kaunti ya Kiambu hii leo limegonga vichwa vya habari baada ya kutangaza kuwa kaunti hiyo inanuia kutumia takriban shillingi milioni 160 kujenga mkahawa na duka litakalotumiwa na wawakilishi wa wadi ya kaunti hiyo katika bajeti yao ya mwaka wa 2018 /2019.
Vile vile takriban shillingi milioni 105 zinapaniwa kutumika kujenga makazi ya spika huku takriban shilingi milioni 80 zikitarajiwa kutumika kujenga eneo la burudani.

Hayo yanajiri huku katika kaunti jirani ya Nyeri ikipendezwa kujengwa kwa nyumba ya gavana Mutahi Kahiga kwa takriban shilingi milioni 200 na takriban shillingi milioni 20 kujenga lango kuu la kaunti hiyo.

Show More

Related Articles