HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Lily Koros aliyesimamishwa kazi ahojiwa na kamati ya afya bungeni

Katika siku ya pili ya mahojiano kati ya kamati ya afya ya bunge na aliyekuwa afisa mkuu mtendaji wa hospiatli kuu ya Kenyatta Lily Koros, sasa imeibuka kuwa kiini cha matatizo yanayokumba hospitali hiyo na haswa Koros huenda kikawa ni zabuni za petroli, maziwa na nyama ambazo chini ya uongozi wake alizitoa kutoka kwa mikono ya watu binafsi hadi kwa serikali ili kupunguza bei.

Kama mwanahabari wetu Grace Kuria anavyotuarifu, suala zima la uchovu kwa upande wa wauguzi liliibuka huku Koros na mkurugenzi wa huduma za kliniki Bernard Githae wakikubali kuwa huenda likawa chanzo cha masihara ya upasuaji yaliyotokea.

Show More

Related Articles