HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Seneta Wetangula ang’atuliwa kama kiongozi wa wachache

Katika hatua inayoashiria uhasama unaotokota baina ya vyama tanzu vya upinzani-NASA, chama cha ODM kimemuandikia spika wa bunge la senate Kenneth Lusaka barua ya kupendekeza kuwa seneta wa Bungoma Moses Wetangula aondolewe kama kiongozi wa walio wachache kwenye bunge la senate.

Kwenye taarifa yake spika wa bunge la senate  Ken Lusaka alasiri ya leo, amedhihirisha kuwa ameafikia uamuzi wa kuondolewa kwa Wetangula kwani muungano wa NASA kupitia chama cha ODM kimeafikia vigezo vinavyohitajika kwa misingi ya kanuni na mwenendo wa bunge.

Show More

Related Articles