HabariPilipili FmPilipili FM News
Shughli Ya Kutafuta Vyeti Vya Kuzaliwa Yazidi Kuwapa Wazazi Tumbo Joto.

Baadhi ya wakaazi hapa mjini Mombasa waendelea kuhangaika wakitafuta vyeti vya kuzaliwa vya watoto wao
Wakizungumza na meza yetu ya habari wengi wao wamelalamikia kutoarifiwa stakabadhi muhimu ambazo wanapaswa kupeleka ili kupatiwa vyeti hivyo.
Wengine wanadai kutoshughulikiwa ipasavyo katika afisi husika, kufuatia msongamano mkubwa unaoshuhudiwa katika afisi hizo, ambapo kufikia sasa wengi bado hawajafanikiwa kupata stakabadhi hizo muhimu.
Shughuli ya wanafunzi kutafutiwa vyeti vyao vya kuzaliwa inatarajiwa kukamilishwa mwishoni mwa mwezi huu.