HabariMilele FmSwahili

Jengo la orofa tano laporomoka mtaani Juja kaunti ya Kiambu

Jengo la orofa tano limeporomoka katika mtaa wa Orion huko Juja kaunti ya Kiambu. Jengo hilo lilikuwa bado linaendelea kujengwa. Hata hivyo hakuna taarifa kuhusu majeruhi. Maafisa wa uokozi wakiwemo wa shirika la msalaba mwekundi wamefika katika eneo hilo. Aidha wapangaji katika majengo yaliyoeneo hilo wamearifiwa kuanza kuhama kufuatia tukio hili.

Show More

Related Articles