HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Wafanyikazi tofauti wahojiwa na kamati ya bunge kuhusu afya

Madaktari wa upasuaji, wauguzi na wahudumu wa afya waliohusika katika upasuaji tata katika hospitali kuu ya Kenyatta hii leo wamefika mbele ya kamati ya afya bungeni na kuhojiwa kuhusu tukio hilo.
Waliofika pia ni familia za wagonjwa wote wawili waliohusika katika masihara ya upasuaji huo huku bodi ya hospitali hiyo ikiagizwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Sabina Chege kujiwasilisha hapo kesho baada ya wengi wao kutofika hii leo kwa madai kuwa walikuwa na shughuli zingine.
Lakini kama mwanahabari wetu Grace Kuria anavyotuarifu, imeibuka kuwa moja ya sababu za masihara hayo ni uchovu kwa wauguzi ambapo siku hiyo walikuwa na wagonjwa wengi wa kuhudumia.

Show More

Related Articles