HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Watoto 3 wafariki Suswa, barabara ya Mai Mahiu yaporomoka

Watoto watatu walifariki kwa kusombwa na maji ya mafuriko huku barabara kuu ya Mai-Mahiu kuelekea Narok ikiporomoka katika eneo la Kirima baada ya mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo.
Wasafiri wanaotumia barabara hiyo walilazimika kutafuta njia mbadala kwani eneo hilo la barabara halingevukika kwa gari wala kwa miguu.
Hata hivyo, tayari matingatinga yamefika eneo hilo kujaribu kurekebisha sehemu hiyo ya barabara.
Dennis Matara alifika maeneo hayo na kutuandalia taarifa hii.

Show More

Related Articles