HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakenya Wapinga Ada Inayotozwa Kupata Kitambulisho Baada Ya Kupotea.

Hatua ya serikali ya kutoza shilingi mia moja kama ada ya kulipia   kitambulisho baada ya kupotea imezua hisia mseto kwa baadhi ya wakaazi  wa Mombasa wengi wakisema  huenda wakashindwa kulipia kutokana hali ya maisha kuwa ngumu.

Baadhi ya tuliozungumza nao  wamekashifu hatua iyo huku wakisema uenda ikaleta ufisadi katika ofisi za serikali hasa zile za huduma centre.

Hata hivyo wengine wameunga mkono hatua hiyo wakielezea kuwa itasaidia pakubwa  watu kuwa waangalifu na kuacha kupoteza vitambulisho ovyo ovyo.

Wapo wengine waliosema kuwa iwapo watalipa shilingi mia moja basi serikali iweze kutoa huduma kwa haraka ili kupata vitambulisho vyao kwa wakati unaofaa.

Hatua iyo ya kulipia shilingi mia moja ili kupata kitambulisho baada ya kupoteza itaanza kutekelezwa hapo kesho.

 

Show More

Related Articles