HabariMilele FmSwahili

Waziri Kariuki : Ugonjwa wa kisukari umechangia asilimia 50 ya vifo barani Africa

Ugonjwa wa kusukari umechangia aslimia 50 ya vifo barani Afrika. Haya ni kwa mujibu wa waziri wa afya Sicily Kariuki anayesema kuwa ugonjwa huo pia umechangia idadi kubwa ya wagonjwa wanaolazwa hospitalini. Kariuki ameeleza haja ya kupelekwa kwa huduma za matibabu katika maeneo ya mashinani na kupunguzwa kwa gharama ya dawa zinazotumika. Kariuki anasema kupitia wizara yake wataimarisha juhudi za kuendesha uchunguzi wa walio na ugonjwa huo maeneo ya mashinani na matokeo kupelekwa katika hospitali zilizo na mitambo ya kisasa ya kushughulikia ugonjwa huo.

Show More

Related Articles