HabariMilele FmSwahili

Mbunge wa Nyali awasilisha hoja bungeni kutaka serikalia kujenga hosipitali ya rufaa kaunti ya Mombasa

Mbunge wa Nyali Mohammed Ali amewasilisha hoja bungeni kutaka serikali kujenga hosipitali ya rufaa kaunti ya Mombasa. Ali anasema kwa mingo kadhaa wenyeji wa Pwani wamesafiri hadi nairobi kupata huduma za matibabu kwa ukosefu wa hospitali ya rufaa kanda ya Pwani. Anasema ujenzi wa hospitali hiyo utawasaidia sio tu wenyeji wa Pwani ila pia kaunti jirani ambazo pia hazina hospitali ya kiwango hicho .Wabunge kadhaa wameunga mkono hoja hiyo,wakielezea haja ya hosipitali za rufaa kujengwa kaunti zote nchini. Kiongozi wa wachache John Mbadi akikiri sekta ya afya imetelekezwa sana na kuna haja ya serikali kuu kushirikiana na zile za kaunti kuiboresha kwa faida ya wakenya wote.

Show More

Related Articles