HabariPilipili FmPilipili FM News

Wanyakuzi Wa Ardhi Waonywa Kwale.

Mbunge wa Kinango kaunti ya Kwale  Benjamin Tayari amewaonya maafisa katika wizara ya ardhi dhidi ya kushirikiana na mabwenyenye,  kunyakua ardhi za umma  akisema atakayepatikana  atakabiliwa kisheria .

Anasema baadhi ya maafisa katika wizara ya ardhi wanajihusisha na maswala ya ufisadi,  akisema wamekua wakigawa ardhi za jamii kwa watu binafsi pasi na wamiliki wa ardhi hizo kujua.

Ameionya jamii dhidi ya uuzaji wa ardhi kiholela, akisema hatua hiyo inasambaratisha juhudi za viongozi,  za kuzuia unyakuzi wa ardhi.

Show More

Related Articles