HabariMilele FmSwahili

Mwanafizikia Stephen Hawking afariki akiwa na miaka 76

Prof Stephen Hawking, mwanafizikia maarufu duniani, amefariki  akiwa na miaka 76, familia yake imetangaza.Mwingereza huyo alifahamika sana kwa kazi yake ya kisayansi kuhusu uwepo wa eneo katika anga za juu ambapo nguvu za mvutano huwa za juu sana kiasi kwamba miali nururishi au hata mwanga hauwezi kuponyoka.Kwa Kiingereza, eneo hilo hufahamika kama ‘Black Hole’.

Alitumia hilo katika kujaribu kufafanua kuhusu asili ya vitu vyote duniani na anganAlikuwa mwandishi wa vitabu kadha maarufu vya sayansi kikiwemo A Brief History of Time (Historia Fupi kuhusu Wakati).

 

 

Show More

Related Articles